Mkutano wa kilele kati ya Muungano wa Afrika na Umoja wa Ulaya – Februari 17 -18 2022: Tamko la asasi za kiraia kwa mustakabali endelevu wa pamoja

African Union-European Union 2022 Summit: Civil society declaration for a common sustainable future

English Version

French Version

Sisi, tunaotia saini, twalikaribisha kongamano la sita baina ya Muungano wa Afrika (AU) na Umoja wa Ulaya (EU) litakalofanyika Brussels, Ujerumani, katika utawala wa urais wa Ufaransa katika Baraza la Umoja wa Ulaya. Kongamano hili ni fursa muhimu ya kuendeleza uhusiano wa karibu baina ya mandugu, na kuunda mustakabali endelevu wa pamoja.`

Tumejitolea kukuza utawala wa kimataifa ili kukabiliana na ukosefu wa usawa, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi, amani na usalama. Utawala wa kimataifa unaofaa utahakikisha kuwa watu wote wanaishi maisha yenye amani, heshima na ufanisi.

Kwa sababu hiyo tunatambua kuwa kuna haja ya dharura ya mbinu za pande nyingi baina ya Afrika na Umoja wa Ulaya. Bara hizi mbili zinakabiliwa na changamoto sawa ikiwamo COVID-19 na mabadiliko ya tabia nchi, na zina maono sawa ya nafasi za pamoja za amani, demokrasia, haki za binadamu, usalama, urafiki na mshikamano. Kwa hivyo, tunatoa wito wa suluhisho za pamoja.

Hali ya hewa na Viumbe hai

Tunatoa wito kwa viongozi kujitolea kuhakikisha sayari yetu haina kaboni angani kufikia mwaka wa 2050. Kufikia mwaka wa 2030, viwango vya mwisho vya uzalishaji wa kaboni zafaa kupungua kwa nusu, na angalau asilimia 30 ya nchi na bahari zihifadhiwe. Umoja wa Ulaya unafaa kuongeza fedha za hali ya hewa kuelekea kwa mataifa ya Afrika ili kutimiza malengo haya. Tunahimiza matumizi ya sarafu ya SDR inayotolewa na shirika la IMF kama mtambo wa kutoa fedha hizo.

Tunadhibitisha kujitolea kwetu kukomesha ongezeko la joto duniani hadi digrii 1.5 ikizidi sana. Tunaunga mkono mapinduzi ya kijani yanayounda kazi, yanayo punguza uzalishaji wa kaboni, na yanayo tumia maliasili kwa njia endelevu na ya kisheria. Kutimiza malengo haya tunahitaji fedha za uboreshaji wa dijitali na kuhama hadi kwa nishati ya kijani. Mabadiliko ya tabia nchi yanahitajika kupewa kipaumbele katika kufanya maamuzi ya kifedha.

Tunatoa wito kwa mkutano huu wa kilele kutambua mabadiliko ya tabia nchi kama tishio lililopo la pamoja kwa mabara ya Afrika na Ulaya, na kuchukua hatua zinazofaa kuhakikisha kuwa eneo jumla la Afrika na Ulaya liko tayari kukabiliana na tishio hili.

Afrika sio eneo la kutupa taka taka. Tunatoa wito kwa mkutano huu wa kilele kuchukua hatua dhidi ya uharibifu wa udongo na matumizi ya maliasili kwa njia isiyo halali.

Demokrasia, utawala wa kisheria, haki za binadamu, na haki

Twaalika mipango ya pamoja yenye lengo la kukuza demokrasia, haki za binadamu, utawala wa kisheria, utawala bora na upatikanaji wa haki. Tunatoa wito kwa mkutano huu wa kilele kueleza kwa ufasaha mbinu ya pamoja ya kimkakati ya ufanisi, uwajibikaji na uwazi wa taasisi, zinazo kamilishwa na kusaidiwa na taasisi za kimataifa na za shirikisho.

Twaomba mkutano huu wa kilele kuendeleza vitendo madhubuti juu ya uhuru wa vyombo vya habari, na mazingira salama ya waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu. Ushiriki wa asasi za kiraia katika maendeleo ya sera na kufanya maamuzi unafaa kuwezeshwa, kwa kuzingatia hasa wanawake na wasichana, vijana, watu wa asili, walio wachache, makundi yaliyo tengwa na watu walio na ulemavu.
Jukwaa la pamoja la AU-EU lipewe jukumu la kukuza maendeleo ya kidemokrasia.

Afya na ubora

Kwa bara zote mbili, COVID-19 imesababisha vifo, imevuruga uchumi na jamii, na imeathiri vibaya haki za msingi za binadamu. Afrika na Ulaya ni sharti washirikiane kurejesha ukamilifu baada ya uhujumu uchumi, wakizingatia Lengo la tatu la Maendeleo Endelevu (Afya na ubora),

Wananchi wanastahili huduma muhimu za afya bora ambazo zinawafikia wote, bila ubaguzi. Mkutano huu wa kilele uhamasishe fedha za umma na binafsi kwa lengo hili.

Mkutano huu wa kilele unafaa kuchukua hatua za dharura za kuongeza kasi ya usambazaji kwa wakati wa chanjo za COVID-19. Usambazaji wa haki wa chanjo hizi ni sharti ili kumaliza janga la COVID-19. Zaidi ya hayo, tunawaalika viongozi kufanya kazi kuelekea hitimisho la Mkataba wa Janga ndani ya Shirika la Afya Duniani.

Amani, Usalama, na Utulivu

Afrika na Ulaya tunapakana katika mazingira ya usalama. Ushirikiano wa ndani zaidi wa usalama na ulinzi baina ya mataifa binafsi, na baina ya bara hizi mbili, ni mwitikio wa kimantiki katika dunia ambayo vitisho vya usalama vinavuka mipaka ya taifa.

Mkutano huu wa kilele unafaa kuchukua hatua za kujenga Shirika la Pamoja la Usalama wa Baharini baina ya Afrika na Ulaya na kuanzisha misheni za jeshi za wanamaji wa EU ili kukabiliana na uharamia na biashara za magendo. Shirika hili litatawaliwa na bunge la pamoja, na litaashiria hatua ya kwanza kuelekea sera za pamoja za usalama.

Elimu, Uhamiaji na Vijana

Kuwasiliana, ubadilishaji, na ushirikiano wa karibu, endelevu na wa mara kwa mara baina ya watu huunda historia za pamoja. Huu ndio msingi wa ushirikiano baina ya bara hizi mbili.

Utafiti, sayansi na uvumbuzi, utamaduni, ziara, mafunzo na elimu ni sekta muhimu za kuhamasisha na kuunganisha watu kupitia maadili ya pamoja, ili kupata maendeleo endelevu ya pamoja na kutengeneza nafasi za ajira, hasa kwa vijana. Tunatoa wito kwa mkutano huu wa kilele kutengeneza Kikundi kimoja cha kufanya kazi kuangazia eneo sawa la utamaduni, kufafanua mipango ya pamoja kama vile elimu ya pamoja, ubadilishaji wa wanafunzi na taaluma na miradi ya ujuzi, miongozo ya historia na jukwaa za vijana.

Ukuaji endelevu

Tumeungana katika kujitolea kwetu kutengeneza ukuaji safi na wa kijani ambao utaunda kazi mpya, bora, na za heshima; kukuza ubunifu; kuongoza uwekezaji katika miundombinu bora; kuimarisha elimu na ustadi wa juu; kukabiliana na ukosefu wa usawa; kulinda mazingira; na kuhakikisha kuwa ustawi wa biashara unafikia sehemu zote za mataifa yetu.

Twakubaliana kuwa kuna haja ya mfumo mpya wa pande zote wa biashara ambao ni wa haki, unao stahimilli, na unaojibu haja za watu wetu. Mfumo huo ni hali ya lazima ya soko wazi, ujumuishaji wa wanawake na vijana, kutetea haki za binadamu na haki za wafanyakazi za kimataifa. Kwa kuzingatia kanuni hizi, Afrika na Ulaya zitachangia utandawazi wa haki na kijani, na ugavi endelevu unaolingana na kanuni elekezi za biashara na haki za binadamu za Umoja wa Kimataifa.

Mkutano huu wa kilele wafaa kutoa hakikisho la mazingira bora ya kufanya kazi, mfumo wa haki wa kodi, uboreshaji wa digitali, uhamiaji wa kijani, na uboreshaji wa mifumo ya ulinzi wa kijamii.

Tunatoa wito kwa mkutano huu wa kilele kuzingatia mikakati ya kufufua uchumi ili kukabiliana na migogoro ya kidunia na mishtuko kama vile janga, ukosefu wa urari katika soko na upotoshaji wa soko.